Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa kwa madai ya kulawiti, kuua

Kulawitiss Akamatwa kwa madai ya kulawiti, kuua

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia mtu mmoja mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka minne na kumsababishia kifo.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 11, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 10, 2021 saa tatu asubuhi huko Chamazi Mbande Wilaya ya Temeke.

Kamanda Muliro amesema uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo unafanyika na hatua za kisheria zitazingatiwa ili haki, itendeke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live