Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa kwa kuiba mtoto wa siku moja amridhishe mume wake

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Mkazi wa  Endakiso wilayani Babati Mkoa wa Manyara, Dori Joshua (20), amekamatwa na mtoto mchanga wa siku moja anayedaiwa kumuiba kutoka kwa Hawa Singai (39).

Dori anatuhumiwa kumwiba mtoto huyo akiwa Bajaji wakielekea katika kituo cha mabasi kwa ajili ya safari kurudi nyumbani wakitokea Hospitali ya Mrara mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Aprili 2, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga amesema mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa alisema  siku ya tukio alifika katika Hospitali ya Mrara, wakati mama mwenye mtoto anaondoka aliomba kumsaidia kwa sababu alikuwa na mizigo mingi.

Amesema mama mwenye mtoto alimpa mtoto mwanamke huyo akiamini ni msamari mwema na kwamba, walipofika kituo cha mabasi alimshauri watumie usafiri wa bajaji ili iwe rahisi kumsaidia kumbebea mtoto wake.

Senga amesema lengo la mtuhumiwa ni kwa ajili ya kumridhisha mume wake ambaye amekuwa akimsumbua muda mrefu anataka mtoto, huku  yeye akiendelea kumdanganya kuwa ni mjamzito na anatarajia kujifungua Machi 31, 2019.

 “Mtuhumiwa aliposhuka njiani alidai anakwenda kutoa fedha ili ziwasaidie wanakokwenda, mama mwenye mtoto alipoona muda unakwenda bila kumuona aliamua kupiga kelele za kuibiwa mtoto.

"Jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi na kijana aliyembeba (Bajaji), tulifanikiwa kumpata akiwa nyumbani kwake Endakiso tayari akiwa amekaa ndani kama mzazi aliyetoka kujifungua,” amesema.

Kamanda huyo amesema katika kufuatilia maeneo hayo vijana walieleza kuwa mwanamke huyo alikodi bodaboda na kukimbia kusipojulikana.

Senga alisema polisi walifuatilia kwa kushirikiana na wananchi na kufanikiwa kumkamata akiwa na mtoto hivyo kumpeleka hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kujua hali ya mtoto.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz