Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akamatwa Mbeya akidaiwa kumiliki mihuri 66 bandia

90673 Mihuri+pic Akamatwa Mbeya akidaiwa kumiliki mihuri 66 bandia

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Polisi Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania limemkamata mkazi wa Isanga mkoani humo akiwa na mihuri bandia 66 ya taasisi tofauti anayoitumia kutengeneza nyaraka za kughushi ili kujipatia kipato kwa njia haramu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei  amesema leo Alhamisi Januari 2, 2020 kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi Jumanne jijini Mbeya baada ya kupata taarifa mtuhumiwa huyo anajihusisha na kuwatengenezea watu nyaraka za kughushi.

Amesema miongoni mwa mihuri hiyo ni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mahakama, Mkuu wa Polisi (OCD) wilaya ya Mbeya, benki za NMB na Access za Mbeya na mingine ni ya  Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya.

“Hii mihuri ameitengeneza kwa maana kwamba atatengeneza ‘Document’ (nyaraka) za ‘ku-forge’ (kughushi) na baadaye akazigonga mhuri halafu zikaenda kutumika vibaya.”

“Tunaendelea kumhoji na baada ya kukamilika kwa uchunguzi tutamfikisha mahakamani. Tunawashukuru sana wakazi wa Jiji la Mbeya kuendelea kutupatia taarifa kwani huyu mtuhumiwa baada ya kupata taarifa zake tulimfuatilia na eneo la Sisimba jijini hapa tuliweza kumkamata akiwa na nyaraka zote hizo,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz