Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajiua baada ya kusoma ujumbe kwenye simu ya mumewe

Ajiua Baada Ya Kusoma Ujumbe Kwenye Simu Ya Mumewe.jpeg Ajiua baada ya kusoma ujumbe kwenye simu ya mumewe

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa Jina la Marietha Bosco Sagana (32) mkazi wa kitongoji cha Matarawe, kijiji cha Marungu kata ya tingi tarafa ya mpepo wilaya ya nyasa Mkoani Ruvuma amefariki Dunia baada ya kunywa sumu chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi.

Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma ACP-Marco Chilya, amesema tukio limetokea Novemba 8,2023 majira ya saa mbili za Usiku, siku ya tukio mume wake alikuwa ameenda shambani lakini alisahau simu yake nyumbani Marietha alivyoiona simu hiyo iliyosahauliwa na mume wake akaanza kuipekua kwa kusoma meseji zote ikiwemo za Whatsapp na akafanikiwa kukuta meseji nyingi za mume wake na mwanamke mwingine.

Marehemu baada ya kusoma meseji hizo alishindwa kuvumilia hivyo akachukua dawa ya kuulia wadudu kwenye mahindi (Actellic) akaikoroga na kuinywa na baadaye Marehemu aliishiwa nguvu majirani walipofika nyumbani kwake na walipomuuliza nini tatizo alisema amekunywa Dawa ya kuulia wadudu kwa sababu ya meseji ambazo amezikuta kwenye simu ya mume wake wakati wanamkimbiza hospital njiani Marietha alifariki Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live