Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajiua baada ya kumuua mkewe, mama mkwe na jirani kwa wivu wa mapenzi

60012 Pic+aua

Tue, 28 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro.  Watu wanne  wakazi wa Dumila mkoani Morogoro wamekufa  akiwemo, Michael Mwandu (54) aliyejiua baada ya kumuua mkewe aliyekuwa na ujauzito wa miezi saba, mkwe wake na jirani yake huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mwandu alifanya mauaji hayo baada ya  kumbana mkewe,  Leonora Ogora (37), aliyekiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine na kisha kueleza waliokuwa wakifahamu jambo hilo ni mama yake mzazi, Magreth Magere (59) na jirani yake, Salma Mkanga(52).

Akizungumza leo Jumatatu Mei 27, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea Mei 25, 2019.

Amebainisha kuwa baada ya Mwandu kuelezwa hayo na mkewe alikoroga sumu na kumnywesha kwa nguvu mkewe na kisha kuchukua panga na kwenda kuwaua Magreth na Salma.

Mutafungwa amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi, akibainisha kuwa polisi walipata taarifa kutoka kwa Salehe Seif ambaye alidai kuwa mkewe Salma alikutwa ameuawa kwa kukatwa na mapanga karibu na nyumba yake.

Kamanda alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliieleza polisi kuwa siku hiyo usiku Mwandu alifika nyumbani kwake na kumuomba Salma akamsaidie mkewe, Leonora ambaye alikuwa mjamzito kwenda kwa mkunga wa jadi na alimruhusu lakini asubuhi alikuta mkewe ameuawa.

Pia Soma

Amesema mtoa taarifa huyo alieleza jinsi alivyoongozana na askari kwenda nyumbani kwa  Mwandu ndipo walipokuta akiwa amekufa kwa kunywa sumu ya mimea iliyokuwa imewekwa kwenye kikombe huku mkewe naye akiwa amekunywa sumu hiyo.

Amesema uchunguzi wa awali wamebaini kuwa mwanaume huyo alinywesha sumu mkewe kwa nguvu  na kisha kumfuata mkwewe ambaye alimkata na panga na kisha kwenda kwa jirani yake na kufanya mauaji pia, kabla ya kurejea tena nyumbani kwake na kunywa sumu aliyomnywesha mkewe.

Amesema mtoto wa wanandoa hao mwenye umri wa miaka 11 alieleza jinsi alivyoshuhudia baba na mama yake wakigombana na alimuona baba yake akitoka na panga.

 “Huyo mtoto alishuhudia mauaji hao na kila kitu kilichokuwa kikiendelea na baba yeke,” amesema Mutafungwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz