Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

Kifo Kifo Mauiaji.png Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Ilula Matalawe Mkoani Iringa, Abel Zakayo Mlasu (26 ) ambaye pia ni Mwigizaji wa Filamu amekutwa amejinyonga kwa kutumia mtandio katika paa la nyumba ambayo alikuwa akiishi yeye na Mama yake huku chanzo kikidai ni ugumu wa maisha uliompelekea kuwa na msongo wa mawazo, Uongozi Mtaa umethibitisha.

Fredy Saimon Nzwaga ni Kiongozi wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Iringa ambaye pia alikuwa ni Mtu wa karibu na Abel ambapo amesema kuwa Abel alikuwa akiishi na Mama yake na kutokana na changamoto za maisha Abel alianza kubadilika na kuanza kunywa pombe na alionekana kama Mtu mwenye msongo wa mawazo.

Elina Mvela ni Mama mzazi wa Abel ambapo amesema October 18, 2023 Mwanae alitoka kwenye mizunguko yake na kurudi nyumbani lakini alikuwa amebadilika sana na kuwa kama Mtu aliyechanganyikiwa na ndipo alichukua hatua ya kumfunga na kamba na kumfungia chumbani na baada ya muda alimuona ametulia na kumpa chakula .

Siku ya tukio Mama mzazi anasema aliamka na kwenda kwenye mizunguko lakini aliporudi nyumbani alikuta Abel amejifungia mlango na ndipo walipofanya juhudi za kuvunja mlango na kukuta amejinyonga kwa kujitundika katika paa la nyumba .

Abel amejingonga October 21,2023 na kuzikwa jana October 22,2023 katika makaburi yaliyopo katika eneo la Ilula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live