Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajinyonga hadi kufa kwa madai ugumu wa maisha

52b5906ce0ad59cdb85cf4871e5a06b2 Ajinyonga hadi kufa kwa madai ugumu wa maisha

Sun, 7 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKAZI wa Kijiji cha Kanazi Kata ya Ntantumbila Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Deus Kakusu (52) amejinyonga hadi kufa, kwa madai ya ugumu wa maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwanampagale amethibitisha mkasa huo ulitokea juzi usiku. Alisema mtu huyo alitumia chandarua cha mbu kujinyonga ndani ya jiko nyumba kwake katika Kijiji cha Kanazi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kanazi, John Kebevage alisema marehemu alichukua uamuzi huo mgumu wakati mke na wanawe wakiwa wamelala.

Alieleza kuwa alfajiri ya siku iliyofuata kulipopambazuka, mke wa marehemu alipotoka usingizini alianza kumuita mumewe, akidhani alikuwa tayari ametoka nje.

Mama huyo baada ya kutosikia mumewe akiitikia, alikwenda jikoni kuwasha moto kuandaa chai, lakini ghafla aliona mwili wa mumewe ukining'inia jikoni humo.

Kamanda Mwanampaghale alisema kuwa mayowe ya mama huyo, yalisababisha taharuki kwa majirani zake ambao walikimbilia eneo la tukio.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kanazi, Given Kisantola alibainisha kuwa marehemu hakuacha ujumbe wote wa maandishi, lakini mara kadhaa alikuwa akisikika akilalamikia ugumu wa maisha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz