Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajinyonga baada ya kukutwa akifanya ngono kwenye kitanda cha baba yake

26091 AJINYONGA+PIC TanzaniaWeb

Fri, 9 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Uganda,Kampala. Mtoto wa miaka 16 amejiua baada ya baba yake mzazi kumkuta akifanya mapenzi chumbani kwake na kijana aliyemtaja kuwa ni mpenzi wake.

Baba mzazi wa mtoto huyo anayeshi Kasenge halmashauri ya Kyengera Kiraka Mugisha, amemkuta mtoto wake huyo akijivinjari kitandani bila wasiwasi kwenye kitanda kilichopo chumbani kwake.

Mugisha alirudi Jumanne  jioni nyumbani  na alipoingia chumbani kwake alimkuta mwanaye huyo aliyemtambulisha kwa jina la Kemigisha akifanya tendo la ndoa  na kijana huyo.

Amesema baada ya hapo aliwachukua mtoto wake huyo na mchumba wake aliyefahamika kwa jina la Kelvin Yunus Kaddu mpaka kituo cha polisi cha Nsangi na kuwafungulia kesi.

Polisi walichukua uamuzi wa kumuachia msichana huyo na kumshikilia mchumba wake Kaddu mwenye miaka 18, kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18.

Mzazi wa Kemigisha aliamua kwenda kwenye duka lake usiku wa Jumanne na aliporudi Jumatano asubuhi alimkuta mwanaye ameshajinyonga akiwa chumbani kwake.

Baada ya tukio hilo aliwaita majirani ambao walitoa taarifa haraka kituo cha polisi ambao walianza uchunguzi mara moja kuhusiana na tukio hilo.

“Ni shetani gani kaingia nyumbani kwangu? Nitamwambia nini  Mungu kwa matukio haya? Ni aina gani ya shetani hili? Nimeisha,” alisema Mugisha huku akiwa anazunguka eneo la nyumba yake.

Msemaji wa Polisi, Luke Owoyesigyire amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema kwamba uchunguzi unaendelea na  kwanza utafanyika uchunguzi wa kidaktari ndio mengine yaendelee.

 “Amesema kwamba hakulala nyumbani alienda kwenye duka lake na aliporudi asubuhi alimkuta mtoto wake ameshafariki kwa kujinyonga na akitumia kamba akiwa chumbani kwake,  ngojea tuchunguze,’’amesema Kamanda Owoyesigyire.

Chanzo: mwananchi.co.tz