Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajifungulia chooni, adaiwa kutupa mtoto

Ajifungua Ajifungulia chooni, adaiwa kutupa mtoto

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa Chamwino, Nasra Khalifa (24) kwa tuhuma za kutupa mtoto mchanga kwenye mtaro baada ya jaribio la kumtumbukiza kwenye shimo la choo cha kituo cha Afya Makole Kukwama.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya mahojiano ya awali alikiri kufanya tukio hilo kutokana na mwanaume aliyempa ujauzito kumkimbia.

Otieno amesema kuwa mtuhumiwa huyo alifika hospitali akidai kusumbuliwa na tumbo baadaye alijifungua chooni na kumuingiza mtoto kwenye sinki.

Kwa mujibu wa Muuguzi wa Kituo cha Afya Makole, Ester Mlinga amesema walimpokea Nasra akiwa ndugu zake na baada ya kusikilizwa shida yake alidai anaumwa tumbo lilimuanza tangu Septemba 12, 2022.

Amesema baada ya kuona ana hali mbaya alipatiwa huduma ya kwanza ya kuwekewa dripu ya maji.

“Baadaye alikwenda chooni na kukaa muda mrefu ndipo tukaingia na wasiwasi na kuanza kugonga mlango muda mrefu lakini hakufungua mpaka baadaye tulipotaka kuvunja mlango alifungua na tulimkuta amejifungua mtoto ambaye alijaribu kumtumbukiza kwenye shimo lakini alishindwa” amesema muuguzi huyo.

Ester amesema mwanamke huyo alijaribu kumuingiza kwa nguvu mtoto huyo ambaye alifanikiwa kuingiza mwili na kukwama kichwa hali iliyosababisha kichanga kupoteza maisha.

Amesema baada ya kumkuta kwenye hali hiyo alipatiwa huduma ya kawaida kama mzazi kwasababu alikuwa kwenye hali mbaya.

Kwa mujibu wa muuguzi ambaye hakutaja jina lake amesema kuwa mwanamke huyo alichukua maiti ya mtoto wake na kutoroka nayo saa 5 usiku

Baadae mtoto huyo aligundulika kutupwa katika eneo la Uhindini jijini humo.

Chanzo: Mwananchi