Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajichimbia kaburi, achoma nyumba zake baada ya kushindwa kulipa mkopo

Chimba Chomaa Ajichimbia kaburi, achoma nyumba zake baada ya kushindwa kulipa mkopo

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja katika Kaunti ya Kisii nchini Kenya amezua kioja baada ya kuchoma nyumba zake na kujichimbia kaburi alilodai kwamba litatumika kumzika yeye pindi atakapofariki.

Imeelezwa kuwa, sasa familia hiyo iliyopo eneo bunge la Nyaribari Masaba Kijiji cha Ibacho sasa italazimika kushinda nje bila makazi baada ya nyumba zote kuchomwa moto na baba huyo.

Inaarifiwa kwamba mwanaume huyo alikuwa na msongo wa mawazo kutokana na mkopo aliouchukua ili kujikimu katika familia yake kufuatia janga la Korona kudhoofisha mapato yao.

Aliposhindwa kustahimili shinikizo kutoka kwa wenye mkopo, alichukua uamuzi wa kutia nyumba zake moto kabla ya kufanya jaribio la kukatisha maisha yake pia ambapo tayari alikuwa amechimba kaburi la kuizika maiti yake.

Msongo wa mawazo ulizidi hata zaidi baada ya sehemu ya ardhi yake kuchukuliwa kama fidia ya mkopo huo, jambo lililomsukuma mzee huyo kuwa mrahibu wa kila aina ya kilevi kama njia ya kujifariji.

Mwanaume huyo alisemekana kuwa mwlimu kabla ya janga la Korona kuingia alichukuwa mkopo ili kuanzisha mradi wa kujenga madarasa ya kuanzisha shule ya kibinafsi sehemu hiyo ila mipango yote ikabuma na mkopo wenyewe walikuwa wameweka hatimiliki ya shamba lake kama dhamana.

Kilichosikitisha wakazi ni kwamba mwanaume huyo alichimba kaburi lake katika moja ya nyumba hizo kabla ya kuziteketeza, lakini kwa bahati nzuri hakufanikiwa kujiua kama alivyokusudia kwani vyombo vya dola viliwahi kwa muda na kumtia nguvuni ambapo alipelekwa katika kituo cha polisi eneo hilo akisubiria kufikishwa mahakamani kwa shtaka la kuharibu mali na kutishia maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live