Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aiba Tsh milioni 19, ahukumiwa kulipa Tsh 150,000

Jela 1.jpeg Aiba Tsh milioni 19, ahukumiwa kulipa Tsh 150,000

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo imemhukumu mshtakiwa Mwinyi Rahabu kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh150,000 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuiba kiasi cha Sh19 milioni  ambazo fedha hizo ni za kaka yake Haji Mwinyi.

Hukumu hiyo imesomwa Aprili 28, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Clauds Kipande alisema mahakama hiyo imemkuta na hatia kwa kuwa mshtakiwa huyo alienda benki ya CRDB tawi la Lumumba na kisha alitoa kiasi cha Sh19 milioni kwenye akaunti ya  Mwinyi kwa nia ya kuiba.

Kipande alisema kutokana na hilo mahakama hiyo imemtia hatiani na imemuhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha miezi sita gerezani au kulipa faini ya Sh150,000 na anaweza kukata rufaa kama hajaridhika na hukumu.

Hata hivyo mshtakiwa huyo ameshindwa kulipa faini hiyo hivyo ameenda gerezani kutumikia kifungo hicho.

Inadaiwa kuwa Desemba 19, 2022 saa 1 usiku mshtakiwa huyo alienda katika benki ya CRDB tawi la Lumumba na kisha alitoa kiasi cha Sh19 milioni kwenye akaunti ya Mwinyi kwa nia ya kuiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live