Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa miaka mitatu jela kwa kuua bila kukusudia

Hukumu Pc Data Ahukumiwa miaka mitatu jela kwa kuua bila kukusudia

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Zainab Muruke amemhukumu Kassimu Joseph adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kuanzia jana Februari Mosi, 2023 baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

Katika shitaka hilo lililosomwa na karani wa mahakama, Asha Salim alisema Mshitakiwa alisomewa mashataka yake katika kikao cha kesi za mauaji namba 41/22 ya kuua bila kukusudia kinyume na kifungu 195 na 198 ya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2019.

Joseph alitenda tukio hilo la kumuua Muksini Namkwacha Agusti 26, 2021 katika kijiji cha Namayakata mkoani humo kinyume na sheria.

Kesi hiyo iliyoendeshwa na mawakili wawili wa Serikali ambao ni Wakili Mwandamizi, Joseph Maugo na Gidion Magessa.

“Nakuhukumu adhabu ya kifungo jela miaka mitatu kuanzia jana kesi hii tumechukua kama mfano unajua mauaji yakitokea wakati watu wanapigana inakuwa ni kuua bila kukusudia lakini tunaangali namna mauaji yalivyofanyika.

“Pia kwenye hii kesi hatujaambiwa marehemu ameacha wategemezi wangapi na watu wangapi wanamlilia nimezingatia hilo lakini pia mshitakiwa hajatusumbua Makahama wala Polisi na hana kumbukumbu ya makosa yoyote ya jinai.

“Sio vitabu vya dini hata Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inakataza na sio sahihi kutoa uhai wa mtu ulipomnyanganya panga ungeweza kukimbia kwenye kesi kama hizi tunaangalia nia ovu sasa wewe kama haukutaka afe kwanini ulikata shingoni hata wanyama tukitaka kuwachinja tunakata shingo” alisema Jaji Muruke

Wakili mwandamizi, Joseph Maugo alioomba Mahakama kuzingatia haki ya kuishi ambayo marehemu ameikosa na kuiomba Mahakama itakapokuwa ikitafakari adhabu ya kumpa mtuhumiwa izingatie haki ya kuishi ya marehemu.

Kwa upande wao mawakili wa upande wa utetezi, Nyachiriga Bright Msalya na Steven Lekey walisema kuwa mshitakiwa alikuwa akijihami ili aweze kujiokoa baada ya marehemu kumtolea panga na kumkata kichwani na mkononi.

“Marehemu alifika nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo alikuwa akimlazimisha dada wa mtuhumiwa kufanya mapenzi, alipoona haitoshi kulazimisha akampiga alipoulizwa kuhusu kumpiga dada wa mshtakiwa na kulazimisha penzi alianza kumshambulia mtuhumiwa kwa panga kichwani na mkononi,” alieleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live