Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa miaka 30 kwa kunajisi

Mbaroni Kwa Mimba Ahukumiwa miaka 30 kwa kunajisi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Wilaya ya Shinyanga imemuhukumu Luhende Heke (80) mkazi wa kijiji cha Ihapa kata ya Old-Shinyanga kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumnajisi mwijukuu wake (8) ambaye alikuwa akisoma darasa la kwanza.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Yusuph Zahoro baada ya kusoma shauri la jinai kesi namba 56 ya mwaka 2023 ambapo alieleza mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 2, 2023 baada ya kutoka shuleni huku bibi yake akiwa shambani.

Hakimu Zahoro amesema kesi ya kubaka chini ya kifungu cha 130 (1)na (2) (e) pamoja na kifungu cha 131( 3) cha makosa ya jinai sura ya 16 kama ilivyorejewa 2022 mahakama imejiridhisha kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye ni mtoto mwenyewe kudai kufanyiwa kitendo hicho na babu yake.

“Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi watatu mtoto mwenyewe alijieleza ,mwalimu shule anayosomea na daktari aliyempima nakujaza PF3 ambapo mahakama imejiridhisha pasipo na shaka kutokana na maelezo na vielelezo vilivyokuwa vikitolewa.’’alisema Zahoro.

Hakimu Zahoro amesema upande wa utetezi wa mshitakiwa alikuwa na mashahidi watano ambapo shahidi wa kwanza ambaye ni mtuhumiwa alisema yeye hakutenda kosa hilo alikuwa kwenye mkutano wa hadhara na mtoto alikuwa akibembelezwa katika kutoa maelezo ya ushahidi.

Hakimu Zahoro amesema shahidi wa pili ambaye ni mke wake na mtuhumiwa alisema alimuona mwijukuu wake akitokwa na damu sehemu za siri alipomuhoji alimueleza alikutana na kijana mmoja ambaye alimuingizia vijiti lakini mume wake hakuwepo nyumbani.

Hakimu Zahoro amesema shahidi wa tatu alidai hakuwepo nyumbani lakini alimuona babu yake akitokea kwenye kikao na shahidi wa nne na tano walieleza mtoto huyo aliwaeleza kuwekewa vijiti sehemu za siri na kijana ambaye hamfahamu ndiyo maana alivuja damu nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live