Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi wa primary

23439 Jela+pic Ahukumiwa miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi wa primary

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kijana aliyefahamika kwa jina la Rwaki Zakaria baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita anayesoma Shule ya Msingi Kigwanhona katika Kijiji cha Kigwanhona Wilayani Uyui na kumsababishia ujauzito.

Katika shauri hilo namba 60 la mwaka 2020 ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Jamhuri, John Nkonyi kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari na Februari mwaka huu kinyume na Kifungu cha 60 cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Ilielezwa Mahakamani hapo kuwa Rwaki ambaye ni mshtakiwa alikuwa akimchukua mwanafunzi huyo wa darasa la sita anayeishi na Bibi yake katika eneo la Kwandanae porini na kumbaka mara kwa mara na kisha kumrudisha nyumbani hadi kufikia hatua ya kumpa ujauzito na kusababisha kukatishwa masomo binti huyo.

Hakimu mkazi katika Mahakama hiyo ya Tabora, Ajali Milanzi baada ya kupitia ushahidi wa watu wanne wa upande wa mlalamikaji na ushahidi uliotolewa na mshtakiwa, Mahakama ilijiridhisha pasipo shaka yoyote kwamba mshtakiwa Rwaki Zakaria amehusika kutenda kosa hilo la jinai na kumhukumu kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka 30 huku ikiacha nafasi kwa mshtakiwa kutafuta haki yake kwa kukata rufaa endapo hataridhika na hukumu hiyo.

MANENO YA WAZIRI JAFO KWENYE MSIBA WA BABA YAKE NA JOKATE

Chanzo: millardayo.com