Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumbaka binti wa miaka 17

70072 Pic+jela.png

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mkazi wa Mwenge mkoani Dar es Salaam Tanzania, Musa Jumanne (23) amehukumiwa adhabu ya kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 jana Jumatatu Agosti 5, 2019 katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni, kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 17.

Akimuongoza mshtakiwa kujibu tuhuma hizo mbele ya Hakimu Anipha Mwingira, Wakili wa Serikali, Hilda Kato alidai kuwa Septemba 20, 2018 shauri lilitajwa kwa Mara ya kwanza, mshtakiwa alidaiwa kumuweka kinyumba na kumbaka binti huyo Julai Mosi, 2018 hadi Julai 21, 2018 eneo la Mwenge Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.

Maelezo ya Bernabetha Kyando ambaye ni mama mzazi wa binti huyo, aliithibitishia mahakama kuwa Julai Mosi, 2018 binti yake alimuaga kuwa anaenda Kanisani, hakurudi nyumbani hadi Julai 2, 2018 binti huyo alituma ujumbe mfupi wa simu akimwambia mama yake, “Miye mzima jamani ila kuna sehemu nipo, nakuja jamani samahani."

Habibu Hassan ambaye ni baba mwenye nyumba wa Musa, aliithibitishia mahakama kuwa alishawahi kumuona Musa akiwa na binti huyo na kutambulishwa kuwa ni mkewe.

Kwa upande wa mshtakiwa, hakuwa na mtetezi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake, hivyo ilimlazimu kujitetea mwenyewe.

Hakimu Mwingira alimuhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha miaka 30 jela kwakuwa upelelezi wa shauri hilo ulikamilika na ushahidi uliotolewa haukuacha shaka yoyote.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz