Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka minne

82480 Kulawiti+pic.png Ahukumiwa maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka minne

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Maiga Maginga (18), amehukumiwa kifungo cha maisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Serengeti baada ya kukiri kumlawiti mtoto wa miaka minne.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 na hakimu mkazi, Adelina Mzalifu baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kulawiti.

Hakimu Mzalifu amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 154 (1) (a) (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Faru Mayengera ameieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 25, 2019.

Amesema alimkuta mtoto huyo akichunga mifugo jirani na nyumbani kwake, alimchukua na kumlawiti.

Amesema mtoto huyo alipiga kelele na mshtakiwa alimuachia lakini alipoulizwa aliyemfanyia kitendo hicho alimtaja mshtakiwa huyo na alipokamatwa alikiri kufanya kitendo hicho. Mayengera amesema hata alipofikishwa katika ofisi ya kijiji na polisi alikiri kufanya kitendo hicho, “pia alipoulizwa na hakimu mara tatu kama amefanya kitendo hiki alikiri.”

Baada ya mshtakiwa huyo kukiri kosa, mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama kutafsiri sheria kulingana na kosa alilotenda.

Chanzo: mwananchi.co.tz