Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa jela miaka miwili kwa kumua mkewe bila kukusudia

Hukumu Pc Data Ahukumiwa jela miaka miwili kwa kumua mkewe bila kukusudia

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Geita imemhukumu kifungo cha miaka miwili Jela, Ivan Denis mkazi wa Kijiji cha Kalema Wilaya ya Chato baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua mkewe Magreth Kinyama bila kukusudia.

Kesi hiyo namba 74/2023 iliitwa kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali ambapo mshtakiwa alikiri kosa la kuua bila kukusudia kinyume na kifungu cha 195 (1) na 198 cha kanuni ya adhabu, kilichofanyiwa marejeo mwa 2022.

Baada ya kukori kosa, Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Kelvin Mhina alimtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, kisha akatoa hukumu. Akitoa hukumu hiyo, jana Februari mosi, Jaji Mhina alisema kwa mazingira ya kesi, uchunguzi wa daktari na utetezi wa mwanasheria wake, mahakama imeona anastahili kupunguziwa muda wa kifungo na hadi miaka miwili jela.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mhina alieleza kuwa Agost 8, 2023, mshtakiwa alichukua fimbo na kumchapa mkewe baada ya kutumia fedha za matumizi alizomuachia kwenda kunywa pombe.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa daktari, mshtakiwa alimchapa marehemu fimbo za mgongoni na kwenye makalio.

Ripoti hiyo ya daktari ilieleza kuwa wakati wa tukio, marehemu alikutwa na ulevi, upungufu wa sukari mwilini uliotokana na kukaa muda mrefu bila kula, pamoja na mshtuko uliotokana na kuchapwa fimbo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live