Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afungwa maisha kwa kulawiti mtoto

45228 Uuajipic Afungwa maisha kwa kulawiti mtoto

Fri, 8 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu kifungo cha maisha jela mkazi wa Stakishari, Ombeni Said maarufu kwa jina la Nyoka (30) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo imetolewa leo  na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Flora Haule.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Haule  amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka Mahakama imeopa pasi na shama mshtakiwa ametenda kosa hilo.

Pia  mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho alimtambua mshtakiwa huyo na ushahidi wa mama mzazi na daktari uliunga mkono hivyo kumuhukumu mshtakiwa huyo kutumikia kifungo cha maisha jela.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono aliiomba Mahakama itoe adhabu inayomstahili  kwa mshtakiwa huyo.

Kwa upande wake mshtakiwa alipopewa nafasi ajitetee kwa nini asipewe adhabu kali, aliomba asipewe adhabu kali kwa sababu anafamilia inayomtegemea.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 560 ya mwaka 2017,  Nyoka anadaiwa alitenda kosa hilo  kinyume cha kifungu cha 154(1)(a) na C cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Oktoba 23, 2017 huko Stakishari wilaya ya Ilala Nyoka alimlawiti mtoto wa kike wa miaka nne. 

Katika kesi nyingine, mkazi wa Ulongoni 'B' wilaya ya Ilala, Sitambuli Siliwa (29) amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulawiti mtoto wa kike wa miaka nane.

Wakili wa Serikali Teddy Mtao alidai mbele ya Hakimu Mkazi Obasi Samwel kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya mwaka 2017 huko Ulongoni B.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana na upande wa mashtaka ulieleza upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hakimu Samwel aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 20 mwaka huu ambapo mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali.



Chanzo: mwananchi.co.tz