Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afungwa maisha jela kwa kumlawiti mtoto wa miaka tisa chooni

Mahakama 2 Afungwa maisha jela kwa kumlawiti mtoto wa miaka tisa chooni

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Wilaya ya Temeke imemuhukumu Mkazi wa Chamanzi, Said Wanie (35) kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Pia mahakama hiyo imemuagiza mshtakiwa huyo kumlipa mtoto huyo fidia ya kiasi cha Sh500,000.

Kati ya Mei 3, 2020 maeneo ya Chamanzi Wilaya ya Temeke mshtakiwa huyo alimlawiti mtoto huyo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi, Anna Mpessa alisema mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyotolewa na daktari vikionyesha kuwa mtoto huyo amelawitiwa.

Mpessa amesema katika ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe ulidai kuwa akiwa maeneo ya nyumbani kwao anacheza mshtakiwa huyo alifika na kumwambia alikuwa anaitwa na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Musa ambaye ni mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Chamanzi.

Amesema mtoto huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa aliongozana mshtakiwa huyo mpaka kwenye choo cha shule hiyo na alipoingia ndani alifunga mlango kisha akamvua nguo na kummwagia maji mwili mzima baadaye alianza kumlawiti .

Mpessa amesema mtoto huyo alidai baada ya kumfanyia vitendo hivyo mshtakiwa aliondoka na kumwacha hapo chooni na alipofika nyumbani alimweleza dada yake kuhusiana na kitendo hicho ambapo naye alimweleza mama yake..

Amesema kutoka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka akiwemo mtoto mwenyewe hakuwa na shaka yoyote hivyo mahakama hiyo ilimtia hatiani mshtakiwa huyo.

"Hivyo mahakama hii inakuhukumu kwenda jela maisha kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka tisa na pia unatakiwa umlipe fidia ya kiasi cha Sh 500,000.

Awali Wakili wa Serikali, Eric Shija aliomba kuwa mahakama hiyo itoe adhabu kali Kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wengine.

Chanzo: Mwananchi