Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afungwa jela maisha kwa kumlawiti mtoto miaka 8

Kortini Pic Afungwa jela maisha kwa kumlawiti mtoto miaka 8

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha na fidia ya Tsh. Millioni 5 Aalon Mveyange kwa kosa la kumlawiti Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 aliyekuwa akisoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Mgongo.

Aalon mwenye umri wa miaka 36 alikuwa akijishughulisha na Kilimo amekutwa na hatia na alikuwa anafahamiana na Mtoto huyo kwasababu alikuwa anaishi Jirani yake.

Akisoma Hukumu Hiyo Hakim Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Aalon aliwakuta Watoto wakicheza akawatuma kwenda kununua pipi kisha akabaki na Binti huyo na kumpeleka chooni kisha kumuingilia kinyume na maumbile.

Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea Aalon aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwasababu ana matatizo ya afya na Mke wake ni mjamzito na muda wowote atajifungua na anategemewa na Familia

Hata hivyo Mahakama ikamuhumu kifungo Cha maisha na fidia ya Tsh. Millioni 5 kwa kosa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live