Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afungwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka sita

Jela Picggggg Afungwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka sita

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imemhukumu Mkazi wa Kijiji cha Kingege Kata ya Malangali, Vicent Christopher Kifwe (21) kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita.

Akizungumza baada ya kutoa hukumu hiyo leo Alhamisi Oktoba 27, 2022 Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Sekela Kyungu amesema kuwa kesi hiyo ya jinai namba 26 ya mwaka 2022 ambayo hukumu yake imetolewa Oktoba 26,2022 katika Mahakama hiyo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Kyungu amesema kuwa Mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 13 mwaka huu huko katika Kijiji cha Kingege Kata ya Malangali baada ya kumchukua mtoto huyo akiwa anacheza na wenzake kuamuru wenzake waondoke kisha kumchukua na kumbaka mtoto huyo.

Hakimu huyo ameeleza kuwa baada mshtakiwa huyo kukana shtaka hilo Mahakama hiyo ilialika upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha shtaka hilo.

" Baada mshtakiwa kukana shtaka la kumbaka mtoto huyo upande wa mashtaka ukaleta mashahidi watatu ambao ni mama wa mtoto, mwathirika ambaye ni mtoto pamoja na daktari kwa ajili ya kuthibitisha shtaka hilo," amesema Kyungu.

Amesema baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka hilo Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo kwa kosa la kumbaka mtoto huyo kwa mujibu wa kufungu 130(1)(2)(e) na 131(3) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 rejeo la mwaka 2022. Hata hivyo hakimu Kyungu amefafanua kuwa Mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo ya kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na jamii wenye tabia kama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live