Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa Mtendajii auawa kwa kukatwa na mapanga ofisini kwake

PANGA Ed Afisa Mtendajii auawa kwa kukatwa na mapanga ofisini kwake

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: Michuzi

Mauaji ya kutisha yametokea eneo la Mbezi Msumi mkoani Dar es Salaam baada ya watu wasiofahamika kudaiwa kuvamia ofisi za Serikali ya Mtaa wa eneo hilo na kisha kumuua Ofisa Mtendaji kwa kumkata na panga.

Tukio hilo la mauaji limetokea Oktoba 11, 2021 kati ya saa sita hadi saa saba mchana wa leo na inadaiwa ofisa huyo mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Msumi ameshambuliwa kwa kukatwa na panga shingoni na watu ambao hawahamiki.

Akizungumza Mmoja wa mashuhuda na mwananchi wa eneo hilo(jina limehifadhiwa) amedai wameshangazwa na tukio hilo la mauaji ambalo limefanywa kwa kiongozi huyo.

Alipoulizwa iwapo watu waliofanya tukio wamefahamika, amejibu hawajafahamika kwani baada ya kutekeleza unyama huo walikimbia na haijulikani ni akina nani na wametoka wapi, ingawa anaamini Jeshi la Polisi linajua namna ya kufuatilia tukio hilo na kuupata ukweli.

"Wananchi tumejawa na taharuki baada ya kutokea tukio hili la mauaji , hatuji nini kimesababisha hadi watu hao kufanya unyama huu kwa kiongozi wa Serikali ya Mtaa,tupo hapa tunasubiri kuona nini kinachoendelea,"amesema shuhuda huyo alipokuwa akizungumza na Michuzi TV

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhan Kingai amethibitisha kupata taarifa hizo za tukio la mauaji na tayari askari polisi tayari wako eneo la tukio."Tumepata taarifa za tukio hilo,tunafuatilia na baadae tutatoa taaria rasmi kwa vyombo vya habari."

Chanzo: Michuzi