Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afikishwa kortini kwa kutoa rushwa Tsh. 300,000

B7b52b0caad304e198a404d8d60bc3ca.jpeg Afikishwa kortini kwa kutoa rushwa Tsh. 300,000

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemkamata mkazi wa Kijiji cha Isenegeja, Kata ya Mwisi katika Wilaya ya Igunga, Richard Masanja (44) na kumfi kisha mahakamani kwa tuhuma ya kutoa rushwa ya Sh 300,000 kwa Katibu wa Baraza la Ardhi.

Masanja ambaye ni mkulima, alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga kwa kutoa rushwa kwa Katibu wa Baraza la Ardhi, Kata ya Mwisi, Philipo Mabula.

Akimsoma shitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Igunga, Juhudi Mdonya, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Wilaya ya Igunga, Mazengo Joseph alidai mshitakiwa alitoa kiasi hicho kama kishawishi cha kupewa upendeleo katika kesi yake ya mgogoro wa ardhi dhidi ya Mhoja Ntima iliokuwepo katika baraza hilo.

Masanja hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo. Kesi iliahirishwa hadi Januari 28, 2022 na mshitakiwa amepelekwa mahabusu baada ya wadhamini kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Chanzo: www.habarileo.co.tz