Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afariki ghafla kwa kula makande na chai (+video)

Video Archive
Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Polisi Mwanza wanachunguza chanzo cha kifo cha Deogratias Meded (42) Mkazi wa Sengerema aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kula makande na chai akiwa kwenye Kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Sengerema kwa Ticketi ya CCM, Hamis Tabasamu ambapo Marehemu alikuwa Meneja wa Kampeni wake.

Polisi Mwanza wanachunguza chanzo cha kifo cha Deogratias Meded (42) Mkazi wa Sengerema aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kudaiwa kula makande na chai akiwa kwenye Kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Sengerema kwa Ticketi ya CCM, Hamis Tabasamu ambapo Marehemu alikuwa Meneja wa Kampeni wake. Kamanda wa Polisi Mwanza Muliro Jumanne amesema “Alifariki dunia ghafla akiwa kwenye msafara wa kampeni, baada ya kula makande na chai alianza kulalamika tumbo linamsumbua, hali yake ilianza kubadilika ghafla na akafariki dunia kabla ya kuanza kupewa matibabu”.

Chanzo: millardayo.com