Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aeleza mahakamani mshtakiwa alivyomshika maziwa

60159 Pic+maziwa

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Temeke ameileza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi mshtakiwa, Finyiasi Didas alivyomshika maziwa wakati akitoka kuoga.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25 ameeleza hayo leo Jumanne Mei 28, 2019 wakati akiongozwa na wakili wa Serikali, Aziza Mhina kutoa ushahidi katika kesi ya jinai namba 237 ya  2019 ya shambulio la aibu inayomkabili mshtakiwa Didas mbele ya Hakimu Mkazi, Frola Mujaya.

Katika ushahidi wake amedai kumfahamu Didas kwa kuwa alikuwa mpangaji mwenzake eneo la Gongo la Mboto Mzambarauni, akibainisha kuwa katika nyumba hiyo kila chumba kinajitegemea .

"Katika nyumba hiyo chumba changu kinafuatana na chumba cha Didas, katika milango kuna makomeo ambayo  tunatumia kufuli na hakuna vitasa wala silingibodi," amesema.

Amedai  Januari 8, 2019 saa nne asubuhi akiwa nyumbani,  Didas aliingia chumbani kwake na kutaka kumbaka.

Amedai siku hiyo ya tukio alitoka kazini usiku na alipofika nyumbani kwake aliingia ndani akalala hadi saa 4asubuhi.

Pia Soma

"Niliamka muda huo nikachukua maji nikaenda kuoga na nilipomaliza wakati  natoka bafuni nikiwa nimejifunga kitenge, Didas aliingia ndani kwangu na kuniambia siku zote ananitongoza namkatalia, akasema kwanini namkatalia wakati yeye pia ni mwanaume,” alidai mwanamke huyo.

Amebainisha kuwa alimueleza Didas kuwa kuna mwanaume  anampenda, lakini mshtakiwa huyo alimjibu kuwa hata mwanaume huyo naye anachepuka.

Amesema licha ya kumueleza maneno hayo, Didas alisema atambaka kwa maelezo kuwa amekuwa akimtongoza lakini anamkatalia.

Baada ya mshtakiwa huyo kuangalia nje na kuona hakuna watu alimtamkia kuwa atambaka, “ Alinivamia kwa kuwa nilikuwa nimevaa kitenge alinibana mikono na kuanza kuchezea chuchu.”

Sharifa amebainisha kuwa alipiga kelele huku akijinasua na baada ya kuona hali imekuwa tofauti, Didas alitoka na kwenda chumbani kwake.

Amesema kutokana na nyumba hizo kutokuwa na silingibodi, alianza kuwasiliana na ndugu zake, mazungumzo ambayo Didas aliyasikia  na kutoka chumbani wake.

“Mimi, wifi yangu na mpangaji mwenzangu mmoja tukaenda kuripoti kwa mjumbe na baadaye polisi Gongo la Mboto.”

"Tangu nimehamia katika nyumba hiyo, Didas alikuwa akinifuatilia, akinitongoza na hata ndugu zangu waliokuwa wakija kunitembelea Didas aliwaeleza kuwa ananipenda lakini mimi nilikuwa namkatalia, “ amesema Sharifa.

Kesi hiyom imeahirishwa hadi Juni 24, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz