Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adanganya kavamiwa na majambazi na kuporwa Mil. 60, yamkuta

Pesa Na Kamanda Adanganya kavamiwa na majambazi na kuporwa Mil. 60, yamkuta

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Deodatus Thadei Luhela maarufu Baba Banzi (35) Mhasibu wa Kampuni ya kichina iitwayo "Your Home Choice" iliyopo Keko kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kituo cha Polisi huku akidai kuwa majambazi walimjeruhi na kumpora Tsh 60,000,000 alizotumwa na Mwajiri wake kuzichukua kutoka Benki eneo la TAZARA.

“Tukio limetokea November 14,2022 eneo la Chang’ombe Temeke ambapo Mtuhumiwa huyo alidai tarehe hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi alikamatwa na Majambazi wawili waliokuwa na gari nyeusi baada ya kumtishia kwa silaha baadae akaingizwa kwenye gari ambapo walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni, na kumpora fedha alizokuwa nazo na baadae kumtupa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi alijikongoja hadi kituo cha Polisi kidogo cha Gongo la Mboto ambako alipewa PF. 3 kwa ajili ya matibabu.

“Baada ya tukio hilo majira ya saa 8:00 mchana Mtuhumiwa huyo alifungua kesi kituo cha Polisi Chang’ombe ya unyang’anyi na kuporwa tsh 60,000,000, Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam walimuhoji kwa kina na kubaini kuwa taarifa hizo zilikuwa ni za uongo na ilipofika tarehe 15/11/2022 majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa aliwaongoza Askri hadi Chanika Kitunguu alipokuwa amezificha pesa hizo.

“Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa Maafisa wa Serikali kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live