Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa na sare za JWTZ, adai alitamani kuwa askari lakini ilishidikana

18113 Pic+adakwas TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kibaha. Mkazi mmoja wa Morogoro anashikiliwa na polisi mkoani Pwani baada ya kukutwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mtu huyo alikamatwa jana baada ya kutiliwa shaka na askari halisi wa jeshi hilo katika eneo la Kwa Mathias mjini Kibaha.

Akizungumzia tukio hilo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafiri kutoka Morogoro kwenda Dar es Salam akiwa amevaa sare hizo.

“Baada ya kutiliwa shaka, askari wa JWTZ kwa kushirikiana na polisi tulimshusha kwenye basi hilo na kumuhoji, alikiri kuwa si  askari wa JWTZ na tulimfikisha kituoni kwa mahojiano zaidi,” alisema.

Kamanda huyo wa polisi alisema akiwa polisi kijana huyo alieleza kuwa sare alizozivaa zilikuwa za babu yake ambaye kwa sasa ni marehemu.

Alisema mtuhumiwa huyo alidai alikuwa anazifaa sare hizo kwa sababu tu ya upendo alionao kwa jeshi hilo na pia  alipenda kuwa askari lakini hakufanikiwa.

“Huyu kijana baada ya kuhojiwa na uchunguzi ukikamilika tutamfikisha mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili kijibu tuhuma dhidi yake,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz