Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa na polisi kwa kujifanya polisi, daktari

67948 Pic+adakwa

Tue, 23 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Rajabu Kambi (23) kwa madai ya utapeli na kujifanya daktari na askari polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 23, 2019 kamanda wa polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema kijana huyo pia amekutwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

“Kwa kuwa alikuwa akivaa sare hizo za polisi walimuamini. Waliotapeliwa ni wapangaji na wenye nyumba, madereva bodaboda waliokuwa wakimpakia kwenye pikipiki na kumzungusha maeneo mbalimbali kisha hawalipi fedha yoyote.”

“Muda wote anakuwa amevaa kofia ngumu kwa sababu alikuwa bado hajapata kofia (ya polisi) na wananchi walimuamini wakidhani ni askari kweli,” amesema Muroto.

Muroto amesema mbali na kushona sare hizo za polisi, kijana huyo alikuwa na bastola bandia na kuna wakati akikuwa akijifanya daktari katika hospitali mbalimbali na kuwatapeli wagonjwa kwa madai atawasaidia kutoa wito kwa hospitali husika wachunguzwe vizuri afya zao.

Amesema watu wenye tabia kama za kijana huyo wanahatarisha usalama wa wagonjwa na kuleta picha mbaya wa hospitali husika.

Pia Soma

Muroto amesema polisi pia wanamshikilia Mussa Pungu kwa tuhuma za kukutwa na  kete 132 za dawa ya kulevya  aina ya heroin.

Chanzo: mwananchi.co.tz