Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa na gunia la bangi!

Suala La Kuhalalisha Kilimo Cha Bangi Sio Jepesi   Kamishna DCEA Adakwa na gunia la bangi!

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limemkamata James Mtewele mwenye umri wa miaka 40 Mkazi wa Kijiji cha Migoli akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi .

RPC wa Iringa, Allan Bukumbi amesema Mtuhumiwa huyo amekamatwa November 17,2023 katika Kijiji cha Nyang’oro Mkoani Iringa akitoka eneo la Ilula kuelekea Kijiji cha Migoli na atafikishwa Mahakamani upelelezi ukikamilika.

Katika tukio jingine Polisi Iringa wamemkamata Edger Mbalanzi ambaye alitoroka Mahakamani akiwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 22/2018 kosa la kupatikana na nyara za Serikali (memory ya Tembo ambaye atatumikia kifungo chake cha miaka 20 jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live