Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa na Mirungi kwenye gari la kubeba maiti

E948f3238216055d770e9091d29a80cb Adakwa na Mirungi kwenye gari la kubeba maiti

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limemkamata mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam Simon Pasian Tarimo(37) akiwa amebeba mirungi bunda 1685 ambazo ni sawa na kilogramu 133 ikiwa imehifadhiwa ndani ya jokofu la kuhifadhia maiti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda amesema gari hilo lilikamatwa jana Januari 12, saa nane usiku huko kwenye Kijiji cha Manga Kata ya Mkata Tarafa ya Mazingira wilayani Handeni.

Chatanda alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha mirungi hiyo akitokea Usangi kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo mbinu iliyotumika ni kuweka mifuko sita aina ya salfeti lenye mirungi kwenye Jokofu linalotumika kuhifadhia Jeneza lenye maiti wakati wa kusafirisha.

Amesema askari waliokuwa doria walilishtukia na walipotaka kulisimamisha dereva akataka kukimbia na wakamkimbiza na kufanikiwa kumkamata na walimuhoji sababu za kukimbia akiwa amesimamishwa na Polisi.

Kamanda huyo amesema baada ya hapo Askari walifanya upekuzi kwenye gari na kukuta kwenye eneo la kuweka mwili kuna mafurushi sita yakiwa yamehifadhiwa mirungi ndani yake na ni eneo ambalo wakati wa kwenda lilikaa Jeneza na wakati wanarudi ndipo walipoweka mirungi.

Kamanda huyo amesema katika mahojiano na dereva huyo alisema baada ya kupelekea mwili Makanya Usangi wakati wa kurudi njiani eneo ambalo aliwekwa maiti akaaamua kuweka mirungi akiamini kwamba angeweza kusafiri salama asipekuliwe kwa sababu anaamini watanzania hawana utamaduni wa kukagua na kupekua magari ambayo yamebeba maiti.

Alilitaja gari la kusafirisha miili ya marehemu ambalo limekamatwa na mirungi hiyo kuwa ni lenye namba za usajili T.569 DSZ aina ya Volvo ambalo ni maalumu kwa kubebea miiili ya marehemu ambalo linamilikiwa na mali ya Nuru Funeral Service iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: habarileo.co.tz