Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa akitorosha dhahabu ya Mil.562.2

Adakwa Akitorosha Dhahabu Ya Mil.562.2.jpeg Adakwa akitorosha dhahabu ya Mil.562.2

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: millardayo

Katika kuhakikisha inalinda rasilimali madini ili ziweze kuchangia maendeleo ya Nchi na kuinua uchumi wa Watanzania, Serikali imesimamisha leseni zote Nchi nzima za Kampuni ya Nadoyoo Mineral Trading kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa Wahusika wa Kampuni hiyo akitorosha dhahabu takribani kilo 4.3 zenye thamani ya zaidi ya Tsh. 562,288,207.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema hayo usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye solo la dhahabu Wilayani Kahama baada ya kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo.

"Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan haitakubali kuona Watu wachache wanajihusisha na vitendo hivi viovu vya kutorosha madini, nataka niwaambie, tutachukua hatua kali dhidi ya yeyote tutakayemkamata akijihusisha na utoroshaji wa madini.

"Ninapoingia Wizara ya Madini mwezi mmoja uliopita nilisema, ukitaka kufahamu sura yangu nyingine basi jaribu kutorosha madini, sasa kuanzia leo mtu yeyote atayekamatwa kwa kosa la kutorosha madini tutakwenda kusimamisha leseni zake zote Nchi nzima wakati tukisubiri hukumu ya vyomvo vya sheria, na iwapo Mahakama itabaini Mhusika ana hatia, tutakwenda kuchukua hatua kali ikiwemo kufuta kabisa leseni zote na kuhakikisha hatajihusisha tena na biashara ya madini nchini"

Chanzo: millardayo