Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa akiiba mtoto Morogoro

Kichanga Pic Adakwa akiiba mtoto Morogoro

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Glory Barnabas (23) Mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kumuiba Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi mitatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama, amesema Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo September mwaka huu ambapo Mtoto huyo aliibiwa kutoka kwa Mama yake ambaye jina lake limehifadhiwa kutokana na kuwa na changamoto ya matatizo ya afya ya akili “Glory alimdanganya Mama huyo kuwa anaenda kumtafutia kazi za ndani Jijini Dar es salaam kisha kumrubuni na kuondoka na Mtoto wake na hata kazi hakumtafutia tena”

"Kimsimgi huyu Mtuhumiwa tulienda kwa lengo la kumkamata kwa matumizi na kuuza dawa ya kulevya lakini baadaye pia tukagundua Mtoto sio wake na tulipomuhoji alikiri kumuiba Mtoto huyo na tayari Mama mzazi amekuja kumchukua na taratibu za kumpima DNA Mama na Mtoto zinaendelea ili kupata uhakika kama ni wake kweli huyo Mama "

“Upelelezi unaendelea na utakapokamilika Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live