Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kuwaua bibi na babu yake arithi mashamba

100978 Bibi+pic Adaiwa kuwaua bibi na babu yake arithi mashamba

Fri, 3 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Emmanuel Kulwa (20), adaiwa kuwaua na kuwazika kisirisiri babu na bibi yake ili apate fursa ya kumiliki na kuuza mashamba yao.

Akizungumza leo Jumatano Aprili Mosi, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Machi 25, 2020  saa 3 usiku katika kitongoji cha kata ya Bukoli wilayani Geita.

Amesema Kulwa anaaiwa kuwaua kwa kuwakata mapanga Donald Machibya (64) na mkewe Ester Kazwenge (60).

Mwabulambo amesema kijana huyo inadaiwa aliunda kundi la vijana kufanya uhalifu huo na walipomaliza kutelekeza aliagiza miili yao kutumbukizwa chooni.

“Tulipata taarifa baada ya wananchi kutilia mashaka kijana huyo kuanza kuuza mashamba na wazee hao kutoonekana,” amesema.

Amebainisha kuwa hawajapata idadi kamili ya wahalifu waliohusika  na tukio hilo, upelelezi unaendelea na kusisitiza kuwa ukweli utajulikana.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz