Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kuuawa kwa kunyongwa, polisi Mtwara wasimulia

Polisi Mtwara Kaimu Kamanda Adaiwa kuuawa kwa kunyongwa, polisi Mtwara wasimulia

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha sinde kata ya Msangamkuu Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa amenyongwa.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Mtaki Kurwijila -ACP amesema marehemu huyo alikutwa akiwa amefungwa kamba ya manila shingoni kama mtu aliyejinyonga.

Amemtaja kwa majina marehemu huyo kuwa ni Samia Mohamed (20), mlemavu wa miguu na mikono ambaye aligundilika amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kufudifudi ukivuja damu mdomoni, puani pembeni mwa jiko nyumbani kwao.

"Katika upelelezi wa awali imebainika kwamba kutokana na ulemavu wa mikono na miguu aliyokuwa nao marehemu, uwezekano wa kujinyonga ni mdogo sana"amesema Kurwijila

Hata hivyo mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Ligula mkoani humo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

"Jeshi la Polisi bado tunaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hili na hadi sasa tunamshikilia mtu mmoja kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio hilo,"amesema

Aidha, imeelezwa kuwa marehemu huyo hadi umauti unamkuta alikuwa akiishi na babu na bibi nyumbani kwao hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live