Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kuua babu yake kwa sime akimtuhumu wizi

65219c378de4f9a9ade5b8bc12fa8865 Adaiwa kuua babu yake kwa sime akimtuhumu wizi

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia mkulima na mkazi wa kijiji cha Mafumbi, kata ya Chole, wilayani Kisarawe, Gale Salaho (32), kwa tuhuma ya kumuua babu yake Haima Nasri (20).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alidai mtuhumiwa huyo alitekeleza mauaji hayo kwa kutumia sime.

Alidai tukio hilo lilitokea Agosti 24, mwaka huu, majira ya saa 11:00 jioni katika kijiji cha Mafumbi.

"Chanzo cha mauji hayo ni kumtuhumu marehemu babu yake kumuibia solar panel," alisema.

Kamanda Nyigesa alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo cha Afya Chole kwa ajili ya uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Chanzo: habarileo.co.tz