Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua rafiki kwa kisu wakicheza muziki

Kisuu?fit=612%2C408&ssl=1 Adaiwa kumuua rafiki kwa kisu wakicheza muziki

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam, Kadi Msela, ameuawa kwa madai ya kuchomwa kisu na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Amir, wakati wakicheza muziki baa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amethibitisha tukio hilo lililotokea Aprili 20, mwaka huu.

Akizungumza nasi, Muliro amesema: “Ni kweli kuna tukio hilo la kijana Kadi kufariki dunia kwa madai ya kuchomwa kisu na rafiki yake Amir. Taarifa za awali zinaeleza kwamba wawili hao walikuwa marafiki na walitofautiana.”

Kamanda Muliro amesema kwa mujibu wa mashuhuda kijana huyo alichomwa kisu sehemu ya shingoni wakati wakicheza muziki katika baa moja iliyokuwa ikizinduliwa eneo la Tegeta.

Ameisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, kwa kumtafuta mtuhumiwa ili hatua zingine za kisheria ziendelee.

Mwandishi wa habari hizi aliyefikia Mtaa wa Uwanja wa Panga lilipotokea tukio hilo na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda, walidai Kadi (marehemu) alikuwa anacheza muziki katika mojawapo ya baa, ghafla rafiki yake alikuja na wakakumbatiana, wakaona Amir anatoa kitu na kumchoma kwenye shingo.

Mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, amesema baada ya mtuhumiwa kutekeleza tukio hilo, alimkalisha kwenye kiti (Kadi) huku akitoka damu na kukimbia.

“Baada ya kumchoma kisu, tulimsikia Kadi (marehemu) akilalamika akisema Amir unaniua? Kisha tukamuona Amir anakimbia kutoka nje ya ukumbi,” amedai shuhuda huyo.

Shuhuda mwingine alidai akiwa ndani ya baa hiyo akicheza muziki aliona kuna purukushani, alipojaribu kufuatilia aliona mtu amedondoka chini na alimtambua kwa jina moja la Kadi ambaye alikuwa akivuja damu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta Wazo, Medard Mashauri, ameiambia Nipashe Digital kwamba kijana huyo (Kadi) ni mwizi na anafahamika mtaani hapo na anayedaiwa kumchoma kisu (Amir) naye anajihusisha na wizi.

Amedai marafiki hao wanakikundi chao wanachokiita panya road, na kifo cha Kadi, marafiki wenzake walikuwa wakipita mtaani na silaha mbalimbali wakitishia wananchi kuwadhuru.

Katika tukio lingine, mkazi wa Tegeta Wazo, Bakari Juma amenusurika kufa maji baada ya kutumbukia katika Mto Tegeta eneo la IPTL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live