Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mwanaye kwa kumchapa fimbo

Fimbo Jkl Adaiwa kumuua mwanaye kwa kumchapa fimbo

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bad News! Mkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaia kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita, kwa kumchapa na fimbo akimtuhumu kuchezea maji.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27 anadaiwa kufanya mauaji hayo Julai 31, 2022, ambapo alimchapa na fimbo sehemu mbalimbali akimtuhumu kuchezea maji ya baridi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa mwanamke huyo tayari anashikiliwa na polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live