Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mtoto wake na kumzika

DEBORAH.webp Adaiwa kumuua mtoto wake na kumzika

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKAZI wa Kijiji cha Sekedidi, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, Lucia Mahazi (42), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kiume wa siku mbili na kisha kumzika, kwa madai ya kutelekezwa na mwanamume aliyempa ujauzito.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea Mei 26, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni.

Alisema wananchi wa eneo hilo waligundua kuwa mwananke huyo hakuwa na mtoto aliyejifungua Aprili 17, mwaka huu na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambalo lilianza kumchunguza na kubaini mtoto huyo alishauawa na mama yake.

"Uchunguzi wa awali ulibaini mama huyo alijifungua mtoto huyo April 17 na kumuua April 19, na kisha kumzika mwenyewe katika eneo la shule ya msingi Ididi wilayani Kishapu, majira ya saa 12 jioni wakati mvua kubwa ikinyesha ili watu wasimuone," alisema Magiligimba.

"Mabaki ya mwili wa marehemu tumeyatoa Mei 26, kaburini na yamekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi, na mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi," aliongeza.

Vile vile, alisema chanzo cha mauaji ya mtoto huyo, ni mtuhumiwa kudai alikabiliwa na ugumu wa maisha, baada ya mwanaume aliyempatia ujauzito kumtelekeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live