Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mpenzi wake kwa wivu

33675 Wivu+pic Tanzania Web Photo

Thu, 27 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Watu wawili wamefariki mkoani Kagera akiwemo Kemilembe Paul (30) aliyepigwa na mumewe hadi kufariki dunia walipokuwa katika matembezi katika Sikukuu ya Krismasi akimtuhumu kuwa alimsaliti.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 27, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema mwanamke huyo aliuawa Desemba 25, 2018 baada ya kuibuka ugomvi baina yake na mumewe walipokuwa katika matembezi katika kijiji cha Kigorogoro wilayani Kyerwa.

Amesema mume wa marehemu, Kamugisha Kadodi (32) anashikiliwa na polisi huku ikidaiwa kwamba kwa muda mrefu mwanaume huyo alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

Amesema katika  tukio jingine Justus Clemence (42) ameuawa na wananchi baada ya kutuhumiwa kuiba kondoo na kumficha kichakani katika kitongoji cha Itokosi wilayani Biharamulo.

Amesema mauaji hayo yametokea jana Desemba 26, 2018 na watuhumiwa wanasakwa na polisi.

Kamanda Malimi amesema baada ya kondoo kupotea wananchi walifanya msako na kumkuta katika kichaka huku marehemu akiwa karibu na eneo hilo na ndipo walipoanza kumshambulia.

“Alifariki wakati akiwa njiani akipelekwa hospitali,” amesema Malimi.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz