Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mama yake kwa kumkata shingo

Kifo Kifo Mauiaji.png Adaiwa kumuua mama yake kwa kumkata shingo

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kikulacho ki nguoni mwako, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada kijana mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa Kijiji cha Lessoroma, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Deogratius Shirima kwa kudaiwa kumuua mama yake mzazi kwa kumkata shingo na kisha kumpasua kichwa na kusababisha ubongo kutoka nje wakati akizuia nyumba yake isibomolewe na kijana huyo.

Tukio la kuuawa kwa mwanamke huyo, Doris Shirima (51) lilitokea Septemba Mosi mwaka huu na kuzua taharuki kubwa kwa wakazi wa Kijiji hicho cha Lessoroma na maeneo ya jirani.

Kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa ni mvutaji bangi kwa mara kadhaa amekuwa akimsumbua mama yake huyo ambaye ni mjane kwa kubomoa nyumba yake anayoishi na kumfanya mama yake huyo kurekebisha nyumba mara kwa mara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea Septemba Mosi mwaka huu na kwamba kijana huyo alimuua mama yake kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali sehemu za shingoni na kichwani na kusababisha kifo chake.

"Ni kweli tukio hili limetokea huko Kijiji cha Lessoroma wilayani Rombo Septemba Mosi saa tatu usiku, mwaka huu huko Kijiji cha Lessoroma ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 26 alimuua mama yake mzazi kwa kumkatakata na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni na kichwani na kusabisha kifo chake," amesema.

Aidha Kamanda Mdogo amesema tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa kuhusika na mauaji ya mama yake.

Mmoja wa majirani na familia hiyo, Pendo Marwa amesema kijana huyo amekuwa na tabia ya kumsumbua mama yake akishavuta bangi na wakati mwingine alikuwa akibomoa nyumba ya mama yake aliyokuwa akiishi kwa mara kadhaa.

Chanzo: mwanachidigital