Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mama yake kwa imani za kishirikiana

Mauaji Abc.jpeg Adaiwa kumuua mama yake kwa imani za kishirikiana

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia kijana Michael Lubinza miaka 20 mkazi wa Kadoto, Kata ya Lyamidati wilayani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua mama yake wa kambo Modest Kadoki aliyekuwa na miaka 67 kwa imani za kishirikiana.

Tukio hilo limetokea Agosti 27 mwaka huu katika kijiji hicho majira ya Saa 6 mchana ambapo kijana huyo inadaiwa alimkuta mama yake huyo sebuleni na kisha kuanza kumshabulia sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia panga hali iliyopelekea kifo chake.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, ACP Leonard Nyandahu akiongea kwa njia ya simu amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitelekeza unyama huo baada ya kumtuhumu mama yake huyo kuwa amekuwa akimuroga na yeye kukosa mafanikio katika maisha na ndipo alipoamua kukatisha uhai wake.

ACP Nyandahu amebainisha kuwa jeshi hilo linamshikilia Kijana huyo ambapo upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kuua kwa kumkata mapanga mama yake huyo wa kambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live