Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kuiba mtoto wa mama mwenye matatizo ya akili

HUKUMU Adaiwa kuiba mtoto wa mama mwenye matatizo ya akili

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Glory Barnabas (23) mkulima na mkazi wa Kata ya Tungi, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za wizi wa mtoto mchanga wa miezi mitatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amesema mwanamke huyo alikamatwa Oktoba 16, 2023 na katika mahojiano alidai mtoto huyo alimuiba Septemba, 2023 kutoka kwa mama mwenye matatizo ya afya ya akili.

“ Huyu mama tulimkamata akiwa na tuhuma nyingine ya makosa ya matumizi ya dawa za kulevya, lakini tukamkuta akiwa na mtoto mdogo wa miezi mitatu …mtoto huyo alikuwa analia sana, hilo likatupa mashaka huwenda akawa sio mtoto wake,” alisema Mkama.

“ … Ni kweli baada ya kufanya naye mahojiano tukagundua huyo mtoto amemuiba na alimuiba tangu mwezi wa tisa mwaka huu na kumfanya ni mtoto wake, “ alibainisha Mkama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live