Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria amchoma kisu kondakta kisa nauli

Kisu.jpeg Abiria amchoma kisu kondakta kisa nauli

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa majina ya Venance Ngonyani mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa mtaa wa Mahenge Manispaa ya Songea kwa kosa la kumchoma kisu kondakta wa daladala anayefahamika kwa majina ya Hussein Anaf (21) mkazi wa Ruvuma Manispaa ya Songea.

Tukio hilo limetokea Februari 25, 2024 katika mtaa wa Mkuzo kata ya Msamala manispaa ya Songea huku chanzo cha ugomvi huo kikidaiwa kuwa ni mtuhumiwa kupanda daladala akiwa na shilingi 500 huku nauli ikiwa ni shilingi 600.

Kitendo ambacho kilipelekea marehemu kumtaka mtuhumiwa kulipa nauli stahiki na kusababisha malumbano baina yao ndipo mtuhumiwa alichomoa kisu alichokuwa amekificha na kumchoma shingoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live