Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilishiaTito Augustino Kiliwa Mkazi wa Mufindi kwa kosa la Kuchapisha kwenye Mtandao wa Facebook taarifa za uzushi kuwa Rais Magufuli anaumwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Rienada Millanzi amesema March 11,2021, kupitia ukurasa wa Facebook, Mtuhumiwa aliandika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaumwa, ujumbe ambao ulileta taharuki ndani ya Jamii.
“Unapozungumzia Kiongozi wa Nchi anaumwa wakati wewe sio mtoa taarifa katika ngazi hiyo hilo ni Kosa lazima tuchukue hatua na baada ya kumfikisha Mahakamni sheria itafuata mkondo wake”– Kaimu RPC Iringa
Mtuhumiwa amekamatwa kupitia kikosi maalum kinachoshughulika na makosa ya mtandao na atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.