Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AKUTWA NDANI YA NYUMBA AKIWA AMESHAFARIKI DUNIA

Bad News?fit=800%2C445 AKUTWA NDANI YA NYUMBA AKIWA AMESHAFARIKI DUNIA

Mon, 9 Nov 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Kijana Mmoja alietambulika kwa jina la Amani  Mohd Omari mweye umri wa miaka 25 amekutwa akiwa ameshafariki dunia katika nyumba yake baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani ambayo ameifunga katika dirisha la choo chake huko Shakani Wilaya ya Magharibi B.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Awadhi Juma Haji amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 7-11-2020 majira ya saa 9:00 usiku huko Shakani.

Ameongeza kusema kuwa  hadi sasa uchunguzi haujabainika kuhusiana na tukio hilo bado wanaendelea na uchunguz wa tukio hilo ilikubaini sababu gani imefanya ajinyonge na kuwataka watu wenye tabia hiyo ya kujinyonga kumuomba mwenyezi mungu kuwaondolea na mawazo hayo mabaya .

Akizungumza na Zanzibar24 Sheha wa Shehia ya Shakani Mwanaisha Khamis Rashid amesema alipokea taarifa kutoka kwa  jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo la kujinyonga kwa kijana huyo na kushirikiana nao kuenda eneo hilo na kuwataka wananchi wanapofika katika shehia wa ripoti taarifa zao kwa viongozi wa shehia ili kuona kwamba panapotokea tatizo iwe rahisi kuwasaidia.

Stor Na Rauhiya Mussa Shaaban.

Chanzo: zanzibar24.co.tz