Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AKATAA KUMPELEKA MZAZI WAKE SHULENI, AMSHAMBULIA MWALIMU WAKE KWA PANGA

Mwalim 1?fit=575%2C396 AKATAA KUMPELEKA MZAZI WAKE SHULENI, AMSHAMBULIA MWALIMU WAKE KWA PANGA

Fri, 25 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mwanafunzi wa Kidato cha tatu Mwita Machamo, (17) wa shule ya sekondari ya Kiagata, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara kwa kumkata na panga mwalimu wake Majogoro John, baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kumpeleka mzazi wake shuleni kama alivyoagizwa na Mwalimu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Daniel Shillah amesema kuwa tukio hilo lilitokea shuleni hapo majira ya asubuhi wakati mwalimu anakagua wanafunzi watoro, na ndipo mwanafunzi huyo alimgeukia mwalimu wake na kumkata mapanga.

“Baadhi ya wanafunzi waliwaleta wazazi wao, lakini huyu mwanafunzi kwa utovu wa nidhamu uliopindukia alikuja na upanga akiwa ameuficha kwenye nguo zake na mwalimu alipohoji kwanini hujaja na mzazi, mwanafunzi akachomoa upanga na kumshambulia mwalimu na akawatisha tisha wanafunzi wengine akapata nafasi ya kukimbia lakini wakamkata na tumemshikilia na atafikishwa mahakamani” Kamanda Shillah

Chanzo: zanzibar24.co.tz