Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA NAILONI

Kitanzi?fit=610%2C374 AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA NAILONI

Mon, 9 Nov 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Suleiman Shaibu Seif mwenye umri wa miaka 27 Mkaazi wa Donge Kipange amefarikid dunia baada ya kujinyonga kwenye muembe kwa kutumia kamba ya Nailoni huko Donge Kipange.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Haji Abdalla Haji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kujinyonga kwa kijana huyo mnamo tarehe 8-11-2020 majira ya saa 12:00 Asubuhi huko Donge Kipange .

Aidha Kamanda haji amesema chanzo cha tukio hilo la kujinyonga bado haijajulikana na maiti imehifadhiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Story na Rauhiya Mussa Shaaban

Chanzo: zanzibar24.co.tz