Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AJINYONGA BAADA YA KUGOMBWA KWA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI KWAO

Kujinyonga?fit=800%2C445 AJINYONGA BAADA YA KUGOMBWA KWA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI KWAO

Sat, 17 Oct 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mwanafunzi mmoja Kijiji cha  Ngayaki wilayani Gairo, Rahel Yohana (14), amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kanga huku chanzo cha tukio hilo kikidaiwa kuwa ni ugomvi kati yake na mama yake mzazi aliyekuwa akimkataza kurudi nyumbani usiku.

Mwanafunzi huyu aliyemaliza darasa la 7 wiki iliyopita katika shule ya msingi Njungwa.

Tukio hilo limedhibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 mwaka huu.

“Aligombezwa na mama yake kwa kosa la kurudi nyumbani mara kwa mara usiku na alitoweka nyumbani na ndipo alipokutwa amejinyoga vichakani, nitoe wito kwa watu ambao wanafikiri ‘shortcuts’ ya changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kuamua kujinyonga, hiyo si sahihi ni bora ukutane na wataalam wa kisaikolojia ili wakusaidie” Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Wilbroad ameongeza kwa kusema watu wanaoona njia ya bora ya kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye maisha ni kukatisha uhai wao, kuwa siyo sahihi na badala yake watafute ufumbuzi wa changamoto zao kwa wataalam.

Chanzo: zanzibar24.co.tz