Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AJIMWAGIA PETROLI NA KUJIWASHA MOTO BAADA YA KUMFUMANIA MKEWE

Capture 144.png?fit=302%2C212 AJIMWAGIA PETROLI NA KUJIWASHA MOTO BAADA YA KUMFUMANIA MKEWE

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Hashimu Selemani maarufu Chikwisu mkazi wa Mtaa wa Julia Newala Mjini Mkoani Mtwara amefariki dunia baada ya kujimwagia mafuta ya petrol mwilini na kujichoma moto huku chanzo cha kufanya hivyo kikidaiwa kuwa ni ugomvi wa kimapenzi.

Akieleza mkasa huo Mtoto wa Marehemu Msafiri Hashimu amesema chanzo cha Baba yake kujiua ni baada ya kumfumania Mkewe na Mchepuko wiki moja iliyopita ambapo baada ya tukio hilo hakuwa sawa hadi kufikia kujichoma moto.

Nae Daktari wa Hospitali ya Ndanda Swaumu Zuberi amesema Hashimu alifikishwa Hospitali akiwa ameungua kwa kiasi kikubwa kuanzia kichwani mpaka maeneo ya tumboni “ tumepambana kumpatia matibabu lakini kwa bahati mbaya amefariki”

Chanzo: zanzibar24.co.tz