Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT wajitokeza wengi kumdhamini Kubenea

KubEentgea ACT wajitokeza wengi kumdhamini Kubenea

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIONGOZI wa Chama cha ACT –Wazalendo wamejitokeza kwa wingi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kumdhamini aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (Chadema).

Viongozi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa ACT Mkoa wa Arusha, Mwahija Choga walisema wamelipa benki Sh 14,546,125, hivyo walikuwa wanasubiri taratibu za mahakama ili Kubenea atoke kwa dhamana.

“Hadi sasa tumeshalipa fedha hizo benki tunasubiri taratibu za kimahakama kumtoa Kubenea “alisema Choga. Alisema nje ya mahakama hiyo kulikuwa na wanachama wengi wa ACT, waliofika kumdhamini Kubenea.

Alisema wanashukuru walilipa fedha ili kufanikisha suala hilo. Awali Kubenea alifikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashitaka mawili, likiwemo kuingia nchini kinyume cha sheria na kuingiza fedha za kigeni bila kutoa tamko kinyume cha Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani za Mwaka 2016.

Kubenea alisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Martha Mahumbuga.

Katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Inocent Njau alidai kuwa Kubenea alikamatwa Septemba 5, mwaka huu katika eneo la Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.

Katika shauri la jinai namba 225 la mwaka 2020, Kubenea anadaiwa kuingia nchini kupitia mpaka usio rasmi akitoka nchini Kenya kinyume cha Sheria ya Uhamiaji Sura 54 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2016.

Katika shitaka la pili Kubenea anakabiliwa na shitaka la kuingiza nchini fedha za kigeni bila kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani za mwaka 2016.

Chanzo: habarileo.co.tz